• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 26, 2013

  CASTLE LAGER WADHAMINI WAPYA BARCA, WAMPA ZAWADI YA JEZI RAIS JK

  Barcelona, Hispania, IMEWEKWA JULAI 26, 2013 SAA 11:22 JIONI 
  BIA ya Castle Lager imeingia makubaliano ya kuidhamini moja ya klabu maarufu zaidi duniani ya FC Barcelona ya Hispania kwa kipindi cha miaka mitatu udhamini utakaokifanya kinywaji hicho kuwa bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika.
  Ushirikiano huu, uliyosainiwa kwenye uwanja wa klabu Camp Nou, unaifanya CASTLE Lager kuwa bia rasmi itakayotumika kwa shughuli yoyote ambayo Barcelona itashiriki kwenye bara la Afrika na pia itafungua milango kwa mashabiki wa Barcelona Afrika kuwa karibu na wachezaji wa Barcelona, vifaa, na kumbukumbu. Pia kupata nafasi ya kusafiri kwenda Hispania kushuhudia kwa karibu timu ya Barcelona.


  Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas akikabidhiwa jezi kwa ajili ya Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Javier Faus, ambaye ni Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia uchumi huko Catalonia Hispania leo hii baada ya kutangazwa kwa udhamini wa Castle Lager kwa Barcelona.

  Mkataba huu utakuwa maalum kwa ajili ya CASTLE Lager kwenye nchi nyingi za Afrika isipokuwa kwa baadhi ya nchi chache zilizochaguliwa ambapo itatumika Castle Milk Stout.
  Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya bara la Afrika. Kushirikiana na bia bingwa Afrika litaongeza kwa haraka umaarufu wa timu ya FC Barcelona ndani ya bara la Afrika na kufungua milango kwa mashabiki wa klabu hii kupata bidhaa mbalimbali za Barcelona na nafasi za kushinda safari ya kwenda Barcelona kuitembelea klabu hiyo.
  “Tumefurahi sana kuingia katika ushirikiano na Castle Lager na Castle Milk Stout, chapa zinayofahamika dunia nzima . Tunafanana na Castle kwa kuwa sote tuna historia ya zaidi ya miaka 100 na utamaduni uliotukuka. Na sote tuna mapenzi na mpira wa miguu pamoja na mashabiki wake katika soko muhimu kama Afrika,” alisema Javier Faus, Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia masuala ya uchumi.
  Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas akimkabidhi zawadi ya asili kutoka Tanzania Bw. Javier Faus, Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia uchumi huko Catalonia Hispania leo hii baada ya kutangazwa kwa udhamini wa Castle Lager kwa Barcelona.

  “Uamuzi wa Barcelona kuingia ushirika na na bia inayoongoza barani Afrika kutaongeza umaarufu wa bia hiyo kwenye bara hili na kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo kufika maeneo amabyo hawajawahi kufika barani Afrika,” alisema David  Carruthers Mkurugenzi wa Masoko wa SabMiller Afrika (kampuni mama ya TBL).
  CASTLE Lager si bidhaa mpya kwenye udhamini wa mpira wa miguu na vyama, ina miaka mingi ya kujihusisha katika soka barani Afrika kwa kipindi cha miaka 85 kupitia ligi mbalimbali za nchi tofauti kama vile Zimbabwe, Swaziland, Botswana, Lesotho na pia mashindano ya kanda kama COSAFA Kusini mwa Afrika na CECAFA Afrika Mashariki.
  Kutokana na soka la Ulaya kupata umaarufu mkubwa na mashabiki wengi barani Afrika, Castle Lager imekuwa ikidhamini urushaji wa matangazo ya ligi hizo kwenye televisheni barani Afrikana kuwapa mashabiki fursa ya kufatilia kila kinachoendelea kwenye ligi hizo maarufu duniani ambazo ni Ligi Kuu ya Ulaya, Ligi Kuu ya Uingereza na La Liga ya Kihispania.
  Kufuatia udhamini huu, wanywaji wa Castle Lager na Castle Milk Stout pamoja na mashabiki wa Barcelona barani Afrika sasa watarajie mambo mengi ya kusisimua katika ulimwengu wa soka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CASTLE LAGER WADHAMINI WAPYA BARCA, WAMPA ZAWADI YA JEZI RAIS JK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top