• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 26, 2013

  STARS MAZOEZINI NAMBOOLE, CHANONGO AMTESA LUHENDE HADI AVUTA JEZI, CHUJI MOTO CHINI

  IMEWEKWA JULAI 26, 2013 SAA 11:34 JIONI
  Safi Chuji; Kiungo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Athumani Iddi 'Chuji' akimtoka Juma Luizio wakati wa mazoezi ya timu hiyo jioni hii Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda, kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji, Uganda, The Cranes. Kushoto ni Kocha Mkuu, Mdenmark, Kim Poulsen na kulia kabisa ni kiungo Frank Domayo.


  Acha jezi wewe; Haruna Chanongo akimtoka David Luhende anayevuta jezi

  Chuji akituliza mpira pembeni ya John Bocco

  Yuko sawa; Juma Kaseja akidaka

  Erasto Nyoni akimtoka Mudathir Yahya

  Ally Mustafa 'Barthez' akidaka mpira aliopigiwa  na kocha wa makipa, Juma Pondamali kulia, huku Juma Kaseja nyuma yake akimuangalia. Mwingine ni Mwadini Ally. Makipa wote wako fiti. 

  Aggrey Morris akimiliki mpira

  Juma Luizio akikokota mpira pembeni ya Chuji

  Kesho watatukoma; Mrisho Ngassa akikumbatiana na Kevin Yondan

  Mwadini Ally akipangua mpira wa juu mbele ya Juma Kaseja 

  Upepo zaidi; Wachezaji wa Stars wakikimbia kuzunguka Uwanja wa Mandela

  Kesho mtalia; Bin Zubeiry katikati akiwa na makocha wa Uganda, Kocha Mkuu Mserbia, Milutin Sredojevic 'Micho' na Msaidizi wake, Mganda Sam Timbe katika baa iliyopo kwenye Uwanja wa Namboole. Uganda walianza mazoezi leo saa 8:30 wakawapisha Stars.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: STARS MAZOEZINI NAMBOOLE, CHANONGO AMTESA LUHENDE HADI AVUTA JEZI, CHUJI MOTO CHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top