• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 26, 2013

  ARSENAL MOTO BATI...YAMALIZA ZIARA YA MASHARIKI YA MBALI KWA USHINDI ASILIMIA 100, KINDA AKPOM AONYESHA NI BALAA

  IMEWEKWA JULAI 26, 2013 SAA 2:53 USIKU
  KLABU ya Arsenal imeondoka Mashariki ya Mbali leo kwa ushindi wa asilimia 100 kwenye mechi zao za kujiandaa na msimu baada ya kupata ushindi mwembamba dhidi ya Urawa Red Diamonds.
  Kinda Chuba Akpom amempa ushindi wa 2-1 kocha Arsene Wenger katika mechi yake ya mwisho kwenye ziara ya Asia.
  Jack Wilshere alianza kwa mara ya kwanza kikosini The Gunners tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo cha mguu Mei, wakati Laurent Koscielny aliyeumia kifundo katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Nagoya Grampus, alianza leo Saitama.
  Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Lukas Podolski dakika ya 48 na Akpom dakika ya 82, wakati la wenyeji lilifungwa na Abe dakika ya 58.
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski; Sagna Koscielny, Mertesacker/Jenkinson dk46, Miquel; Arteta/Rosicky dk46, Wilshere/Ramsey dk46, Oxlade-Chamberlain/Zelalem dk67, Walcott/Akpom dk75, Gnabry/Miyaichi dk46, Giroud/Podolski dk46. 
  Urawa Reds: Yamagishi; Tsuboi, Nasu, Abe, Ugajin; Kojima, Kashiwagi, Umesaki, Richardes; Yamada na Koroki Subs.On target: Lukas Podolski (left) struck the opener for Arsenal against the Red Diamonds
  Lukas Podolski (kushoto) alifunga bao la kwanza kwa Arsenal dhidi ya Red Diamonds
  How about that? Chuba Akpom celebrates after earning Arsenal the victory
  Chuba Akpom akishangilia bao lake la ushindi
  Taken out: Yuki Abe and Theo Walcott clash during the friendly
  Yuki Abe na Theo Walcott 
  We believe in Boss: Arsene Wenger is shown support by these fans in Saitama
  Mashabiki wakionyesha sapoti kwa kocha Arsene Wenger mjini Saitama
  Olivier Giroud
  Serge Gnabry
  Olivier Giroud (kushoto) na Serge Gnabry (kulia) 
  Backing: Walcott had a mixed game but these fans loved him
  Sapoti kwa Walcott kutoka kwa mashabiki
  Mexican wave: Japanese Arsenal fans enjoy themselves prior to the pre-season friendly match
  Mashabiki wa  Arsenal Japan wakifurahia mechi leo
  All together now: Arsenal players show off a banner after the game
  Wachezaji wa Arsenal wakionyesha bango baada ye mechi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL MOTO BATI...YAMALIZA ZIARA YA MASHARIKI YA MBALI KWA USHINDI ASILIMIA 100, KINDA AKPOM AONYESHA NI BALAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top