• HABARI MPYA

    Friday, July 19, 2013

    VILANOVA AACHIA NGAZI BARCELONA BAADA YA HALI YA AFYA KUWA MBAYA, NAFASI YAKE KUPEWA MSAIDIZI WAKE RUBI

    IMEWEKWA JULAI 19, 2013 SAA 2:17 USIKU
    KLABU ya Barcelona imeitisha Mkutano na Waandishi wa Habari saa 3:30 usiku wa leo kwa saa za Uingereza wakati wanatarajiwa kutangaza kwamba kocha Tito Vilanova ameachia ngazi.
    Mwalimu huyo mwenyr umri wa miaka 44, ambaye amekuwa akitibiwa saratani, amelazimika kuachia ngazi baada ya hali kuwa mbaya.
    Tito Vilanova speaks to his players during a training session on Thursday
    Anaaga? Tito Vilanova akizungumza na wachezaji wake katika mazoezi ya jana

    Vilanova alirithi mikoba ya Pep Guardiola msimu uliopita, lakini alikosa sehemu kubwa ya msimu baada ya kwenda kutibiwa saratani Marekani. 
    Katika msimu wake wa kwanza kazini akirithi mikoba ya kocha aliyefanikiwa zaidi, aliiwezesha klabu kurejesha ubinga wa Ligi kutoka kwa wapinzani, Real Madrid.
    Rais wa Barca, Sandro Rosell na Mkurugenzi wa Michezo, Andoni Zubizarreta wanatarajiwa kuthibitisha kung'atuka kwa Vilanova katika mkutano wa usiku huu.
    Msaidizi wa Vilanova, kocha wa zamani wa Girona, Joan Francesc Ferrer 'Rubi', anatarajiwa kuteuliwa kocha wa muda wa dharula, wakati klabu ikitafuta kocha wa kudumu.
    Ill health: Vilanova has suffered a relapse
    Afya mgogoro: Vilanova anasumbuliwa na afya
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: VILANOVA AACHIA NGAZI BARCELONA BAADA YA HALI YA AFYA KUWA MBAYA, NAFASI YAKE KUPEWA MSAIDIZI WAKE RUBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top