• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 24, 2013

  PIGO JUU YA PIGO ARSENAL, HIGUAIN ATUA NAPOLI KWA DAU LA PAUNI MILIONI 32

  IMEWEKWA JULAI 24, 2013 SAA 7:59 MCHANA
  KOCHA Arsene Wenger anakabiliwa na presha ya kuwasajili Luis Suarez au Wayne Rooney, baada ya mchezaji aliyekuwa anamtaka zaidi Gonzalo Higuain kukubali kuhamia Napoli kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 32.
  Higuain alikuwa anatakiwa sana Arsenal ili kuwafariji mashabiki wa timu hiyo na alikuwa pia akitakiwa na Liverpool katika mpango wa kubadilishana wachezaji na Suarez.
  Lakini wakati Arsenal ikihangaikia bei ya mchezaji huyo Real Madrid, Napoli imepiga hatua na fedha mbele na kufanikiwa kumnasa kiulaini. 
  Italian job: Gonzalo Higuain has signed for Napoli
  Kazi Italia: Gonzalo Higuain amesaini Napoli
  Wametoa ofa ya Pauni Milioni 31.8 Real na Higuain atasaini Mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki.
  Mshambuliaji huyo wa Argentina sasa anakwenda Uwanja wa San Paolo kuziba pengo la Edinson Cavani aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 55 na Paris St Germain na kufanya kocha mpya wa Napoli na wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez ajivunie kupata kifaa cha maana.
  Not Gunner move: Higuain has turned down a move to Arsenal and opted for Napoli
  Ameukataa mtutu: Higuain amekataa kwenda Arsenal na kuamua kutua Napoli

  Wenger sasa atatakiwa kuongeza nguvu katika harakati za kumng'oa Suarez Anfield au kupambana na Chelsea kuwania saini ya mshambuliaji asiyefurahia maisha Manchester United kwa sasa, Rooney.
  Swapping Spain for Italy: Higuain has joined Napoli for £1.8m
  Kutoka Hispania hadi Italia: Higuain amejiunga na Napoli kwa Pauni Milioni 31.8.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: PIGO JUU YA PIGO ARSENAL, HIGUAIN ATUA NAPOLI KWA DAU LA PAUNI MILIONI 32 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top