• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 31, 2013

  MAN UNITED WAPELEKA OFA YA TATU BARCELONA, NI HAIJAWAHI KATIKA HISTORIA YA KLABU

  IMEWEKWA JULAI 31, 2013 SAA 8:52 MCHANA
  KLABU ya Manchester United inajianda kuvunja rekodi yake ya usajili kwa kutuma ofa ya mwisho ya Pauni Milioni 35 kwa Barcelona ili kumsajili Cesc Fabregas.
  Kiungo huyo wa Hispania ni mlengwa mkuu wa David Moyes kocha huyo mkuu wa United akitazamiwa kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu. 
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu England wamekuwa kwenye majadiliano na Barcelona kwa wiki kadhaa, huku ofa za awali za Pauni Milioni 26 na Milioni 30 zikipigwa chini na klabu hiyo ya Katalunya.
  Change the record: Cesc Fabregas is top of Manchester United's transfer list and they are prepared to break their transfer record with a third bid
  Kubadili rekodi: Cesc Fabregas ni mlengwa mkuu katika usajili wa Manchester United ambayo sasa inajiandaa kupeleka ofa ya tatu
  Spain game: Cesc Fabregas is top of Manchester United's transfer list, but he is unlikely to be sold

  REKODI ZA USAJILI UNITED

  Roy Keane (Nottingham Forest, £3.75m - Julai 1993)
  Andy Cole (Newcastle, £7m - Januari 1995)
  Jaap Stam (PSV, £10.75m - Julai 1998)
  Dwight Yorke (Aston Villa, £12.6m - Agosti 1998)
  Ruud van Nistelrooy (PSV, £19m - Julai 2001)
  Juan Sebastian Veron (Lazio, £28.1m - Julai 2001)
  Rio Ferdinand (Leeds, £30m - Julai 2002)
  Dimitar Berbatov (Tottenham, £30.75m - Septemba 2008)
  (£, maana yake Pauni)
  Sasa, United inajiandaa kurejea na dau la Pauni Milioni 35, ambalo litapiku dau la Pauni Milioni 30.75 ambazo kocha Sir Alex Ferguson alitoa kumnunua Dimitar Berbatov mwaka 2008. 
  Hadharani, Barca wanaendelea kusistiza Fabregas hatauzwa na kocha mpya Gerardo Martino amesema: "Siwezi kujihusisha na akaundi za klabu, lakini kwa kuzingatia klabu imekwishakataa ofa mbili, naweza kuhisi na ofa ya tatu nayo pia itakataliwa,".
  BIN ZUBEIRY inafahamu Fabregas amewaambia rafiki zake atafungua uwezekano wa kujiunga na United na yuko tayari kuungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie.
  Cesc Fabregas
  Fighting the cause: David Moyes has already seen two bids turned down for the Barcelona man
  Anapambana: David Moyes amekwishatoa ofa mbili zimepigwa chini Barcelona
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED WAPELEKA OFA YA TATU BARCELONA, NI HAIJAWAHI KATIKA HISTORIA YA KLABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top