• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 21, 2013

  SPURS YASAJILI BONGE LA WINGA LA UBELGIJI LENYE ASILI YA MOROCCO

  IMEWEKWA JULAI 21, 2013 SAA 2:15 USIKU
  KLABU ya Tottenham Hotspur imenasa wa Kibelgiji, Nacer Chadli kwa dau la Pauni Milioni 6 kutoka FC Twente.
  Chadli, mwenye umri wa miaka 23 ambaye anaweza kucheza pembeni pande zote, ataungana na Wabelgiji wenzake, Mousa Dembele na Jan Vertonghen iwapo atakubali Mkataba wa miaka mitano kama inavyotarajiwa.
  Klabu hiyo imethibitisha Chadli ataungana na kikosi kwa ajili ya maandalizi ya msimu kwenye kambi ya Hong Kong baada ya kufuzu vipimo vya afya na kukubaliana na vipengele vya Mkataba.
  Swoop: Tottenham have confirmed the signing of Nacer Chadli from FC Twente for £6million
  Kanaswa: Tottenham imethibitisha kumsajili Nacer Chadli kutoka FC Twente kwa Pauni Milioni 6

  Usajili wa winga huyo ni zawadi nzuri kwa kocha wa Spurs, Andre Villas-Boas, ambaye atapenda kumtumia mchezaji huyo pamoja na nyota wake wa mabao, Gareth Bale uwanjani. 
  Alifunga bao Uwanja wa White Hart Lane katika Ligi ya Mabingwa wakati Tottenham ilipopangwa kundi moja na Twente miaka mitatu iliyopita.
  Swansea na Aston Villa pia zilionyesha nia ya kumsajili Chadli, ambaye uraia wa pili na aliichezea Morocco mechi ya kirafiki, kabla ya kuamua kufuata uraia wa nchi aliyozaliwa, Ubelgiji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SPURS YASAJILI BONGE LA WINGA LA UBELGIJI LENYE ASILI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top