• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 23, 2013

  ARSENAL WAZIDI KUMPANDIA DAU SUAREZ, WENGER ULIMI NJE KWA NYOTA WA URUGUAY

  IMEWEKWA JULAI 23, 2013 SAA 4: 37 USIKU
  KLABU ya Arsenal imeendelea na harakati za kuwania saini ya msahmbuliaji wa Liverpool, Luis Suarez.
  Arsene Wenger anaamini mchezaji huyo mwenye kipaji kutoka Uruguay ataisaidia Arsenal katika Ligi Kuu ya England na anataka kuvunja rekodi ya usajili ya klabu yake kwa kutoa Pauni Milioni 40.
  Dau la Pauni Milioni 40 linaweza kuwa sawa kwa Suarez, lakini inafahamika Arsenal itatoa kwanza Pauni Milioni 35 na nyingine Milioni 7 saba watalipa kwa vipengele, maana yake hakuna namna ambayo Liverpool watakubali.
  Fresh bid: Luis Suarez could yet leave Liverpool before the end of the season
  Ofa ya mafungu: Luis Suarez yuko tayari kuondoka Liverpool kabla ya mwisho wa msimu
  Ofa za awali za Pauni Milioni 30 na Milioni 35 tayari zimepigwa chini na Liverpool, ambayo ilimnunua kwa Pauni Milioni 22.7 Suarez Januari mwaka 2011, lakini Arsenal imemfanya mchezaji chaguo la kwanza katika inayowahitaji baada ya jithada zao za kumnasa Gonzalo Higuain kueleeka kukwama.
  Rekodi ya Arsenal kusajili mchezaji kwa bei kubwa ni Januari mwaka 2009, ilipolipa Pauni Milioni 15 kumnunua Andrey Arshavin. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL WAZIDI KUMPANDIA DAU SUAREZ, WENGER ULIMI NJE KWA NYOTA WA URUGUAY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top