• HABARI MPYA

  Alhamisi, Julai 25, 2013

  MAN UNITED MTEGONI...VALENCIA YAWASILISHA MAOMBI YA KUMCHUKUA CHICHARITO AKAFUFUE MAKALI HISPANIA

  IMEWEKWA JULAI 25, 2013 SAA 3:14 ASUBUHI
  KLABU ya Valencia inamtaka mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez maarufu kama Chicharito kwa mkopo.
  Klabu hiyo ya Hispania imeandaa orodha fupi kusaka mchezaji wa kuziba pengo la Roberto Soldado ambaye anakaribia kujiunga na Tottenham, lakini pia anatakiwa na Liverpool.
  Valencia imeweka bajeti maalum na hiyo inahusisha pia mshambuliaji kinda wa Manchester City,John Guidetti.
  Target: Valencia want to bring Javier Hernandez to Spain to replace their departing striker
  Anatakiwa: Valencia inamtaka Javier Hernandez ahamie Hispania kuziba pengo la mshambuliaji wake anayetaka kuondoka
  Incoming: Roberto Soldado is a target for Tottenham and Liverpool
  Anaondoka: Roberto Soldado anatakiwa na Tottenham na Liverpool

  Pamoja na hayo, wanaamini wanaweza kumpata Hernandez kwa sababu kwa sasa hana namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu.
  Mshambuliaji huyo wa Mexico amekuwa hatumiki sana kwa miezi 18 iliyopita, kufuatia kuwasili kwa Robin van Persie. Pia amekuwa akijadiliwa na Atletico Madrid na Juventus katika miezi ya karibuni, lakini amerudia kusema anataka kubaki Old Trafford.
  Kocha David Moyes ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na haitakuwa rahisi kumruhusu kuondoka, hususan kutokana na kwamba United bado haijasajili mchezaji mwenye jina kubwa inamyemtaka.
  Mustakabali wa Wayne Rooney pia unachangia, United inapambana kumzuia mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kumzuia kuhamia kwa wapinzani Chelsea na Arsenal.
  Big fan: David Moyes likes Hernandez and will be reluctant to let him leave
  Shabiki mkubwa: David Moyes anampenda Hernandez na haitakuwa rahisi kumruhusu kuondoka
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED MTEGONI...VALENCIA YAWASILISHA MAOMBI YA KUMCHUKUA CHICHARITO AKAFUFUE MAKALI HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top