• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 31, 2013

  SIMBA SC YASAJILI STRIKER LA MAREKANI JIONI HII


  IMEWEKWA JULAI 31, 2013 SAA 12:03 JIONI
  Mshambuliaji wa zamani wa Pamba FC ya Mwanza, Betram Mombeki (kulia) aliyekuwa Marekani kwa muda mrefu, akisaini Mkataba wa miaka miwili kuichezea SImba SC leo, baada ya kuvutia katika majaribio. Kulia ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang'are 'Kinesi'.
  Kama Yekini; Betram alifunga bao zuri Simba SC ikilala 2-1 dhidi ya URA mwezi huu na kushangilia kwa staili ya mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, marehemu Rashid Yekini (chini). Lakini siku hiyo alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko beki wa URA.

  Anaweza; Betram alionyesha uwezo mkubwa dhidi ya URA na kama si kutolewa kwa kadi nyekundu, angeweza kufunga zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI STRIKER LA MAREKANI JIONI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top