• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 20, 2013

  MAN UNITED YA MOYES YAFUNGULIA MBWA...YAUA 5-0

  IMEWEKWA JULAI 20, 2013 SAA 5:35 USIKU
  MICHEZO ya kujiandaa na msimu, wakati yote yamesemwa na yamefanyika, inatumika kutengeneza fedha na kuimarisha timu. 
  Pamoja na hayo, inaweza kuwasaidia kuwajengea kujiamini pia, mfano Danny Welbeck atakwenda Japan na Manchester United wiki hii akiwa katika hali nzuri kimchezo.
  Kocha wa United, David Moyes amesema mjini Sydney kwamba anafikiri anahitaji kuketi chini na Welbeck katika hoteli ya timu wiki hii na kuzungumza naye kinda huyo wa kimataifa wa England mambo muhimu anapokuwa mbele ya lango. 
  Boost: Danny Welbeck's two goals will help his confidence going into the new season
  Danny Welbeck amefunga mabao mawili leo
  Impressive: Youngster Jesse Lingard scored twice in an excellent performance
  Jesse Lingard amefunga mabao mawili pia 

  Akiwa amefunga mabao mawili tu msimu uliopita mambo yanaelekea kubadilika sasa.
  Kwenye Uwanja wa ANZ leo, Welbeck alifanya vitu adimu, akifunga mabao mawili katika dakika za 34 na 71 na kuwa mwiba mchungu kwa walinzi wa A-League All Stars kwa dakika zote 70 alizokuwa uwanjani.
  Mabao mengine ya Mashetani hao Wekundu yalifungwa na Jesse Lingard mawili pia dakika za 11 na 55, mshambuliaji tegemeo zaidi wa timu, Robin Van Persie dakika ya 87.
  Bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Berisha dakika ya 52.
  Kikosi cha Man Utd kilikuwa: Lindegaard, Rafael, Ferdinand/Keane dk46, Jones, Evra, Zaha, Carrick/Anderson dk71, Cleverley, Lingard, Giggs/Van Persie dk62 na Welbeck/Januzaj dk71.
  All Stars: Covic, Bojic, Beauchamp, Boogaard, Topor-Stanley, Rose, McGlinchey/Grant dk62, Emerton/Carrusca dk84, Miller, Broich na Berisha.Maiden: New boss David Moyes celebrated his first win in charge of the club
  Kocha mpya, David Moyes ameshangilia ushindi wake wa kwanza tangu aanze kazi
  One back: Besart Berisha celebrates making it 2-1
  Besart Berisha akishangilia bao lake lililofanya mchezo uwe 2-1
  At the double: Lingard is mobbed after scoring an excellent second goal
  Lingard akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao zuri la pili
  Late goal: Robin Van Persie adds a fifth in the dying minutes
  Robin Van Persie alifunga la tano dakika za lala salama
  Impressive: Lingard had an excellent match 
  Clearance: United skipper Patrice Evra heads the ball away
  Nahodha wa United, Patrice Evra akiondosha mpira hatarini kwa kichwa 
  In the spotlight: Wilfried Zaha was also impressive for United
  Wilfried Zaha pia alivutia United
  Huge support: 80,000 fans turned up to watch the match
  Mashabiki 80,000 walikuwa uwanjani leo
  Tussle: Ryan Giggs does battle with Nikolai Topor-Stanley
  Ryan Giggs akipambana na Nikolai Topor-Stanley
  Strike: Thomas Broich shoots at goal for the All Stars
  Thomas Broich akipiga shuti 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED YA MOYES YAFUNGULIA MBWA...YAUA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top