• HABARI MPYA

    Monday, July 22, 2013

    YANGA NA AZAM KUWANIA NGAO AGOSTI 17 TAIFA, LIGI KUU KUANZA AGOSTI 24

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JULAI 22, 2013 SAA 6:10 MCHANA
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14 kuwa viwanjani katika miji saba tofauti.
    Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Inavyokuwaga; Yanga na Azam katika mechi ya Ligi Kuu msimu uliopita

    Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
    Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).
    Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani. (Ratiba ya mzunguko wa kwanza na wa pili imeambatanishwa- kulia angalia).

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA NA AZAM KUWANIA NGAO AGOSTI 17 TAIFA, LIGI KUU KUANZA AGOSTI 24 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top