• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 31, 2013

  BALE AAMUA KAMA NOMA NA IWE NOMA, AMUAMBIA VILLA BOAS USO KWA PUA; "NAONDOKA ZANGU"

  IMEWEKWA JULAI 31, 2013 SAA 3:11 USIKU
  NYOTA Gareth Bale amempasukia usoni Andre Villas-Boas na kumwambia kwamba anataka kuondoka Tottenham na kujiunga Real Madrid wakati huu wa kiangazi.
  Taarifa hii ni mbaya kwa Tottenham hasa ikiwa hii ni siku ya kwanza ya staa huyo wa Wales kwenye mazoezi ya klabu hiyo, baada ya ofa ya pauni milioni 85 kuwekwa mezani na miamba hiyo ya Hispania.
  Mkurugenzi wa Michezo wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kwamba Bale anastahili kuachwa kutimiza ndoto yake ya kujiunga na Real Madrid, na kuongeza kwamba anaweza kuwa mchezaji bora wa dunia kama akitua Bernabeu.
  Heading in: Gareth Bale returned to Tottenham training on Wednesday morning
  Anaondoka: Gareth Bale amemwambia kocha wa Spurs, Andre Villas-Boas kwamba anataka kuondoka
  Inbound: The Welsh star, who wants to move to Spain, arrived at training on Wednesday morning
  Ndani: Bale akiwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Spurs jana asubuhi 
  Heading in: Bale pictured leaving his house this morning
  Heading in: Bale pictured leaving his house this morning
  Anatoka: Bale akiondoka nyumbani kwake Essex, Jumatano asubuhi na kwenda mazoezi Tottenham 

  Straika wa Wales anataka kuondoka, lakini hataki kuweka mezani maombi rasmi ya kuondoka Tottenham. 
  Msimu uliopita alipata tuzo zote mbili ya Mchezaji Bora wa Kulipwa na ile ya waandishi wa habari na tayari anatajwa kama mmoja kati ya wachezaji bora duniani.
  Spurs wameshangazwa na mabadiliko ya ghafla ya Bale, 24, tangu Real walipolivalia njuga suala lake.
  Ni wiki iliyopita tu walikuwa wakiamini kwamba atasaini mkataba mpya na uhusiano wake mzuri na Andre Villas-Boas utamshawihi kubaki.
  Lakini hiyo ilikuwa kabla ya Real hawajamfungulia Zidane, ambaye alisema kwamba siyo ajabu kwa mchezaji kuchachawa akisikia kwamba anatakwa na Real Madrid kwa sababu ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa jezi nyeupe za Real Madrid.
  Huku akiongeza kuwataka Spurs wamuache Bale akae meza moja na Real wazungumze kwa sababu nafasi kama hiyo huja mara moja tu maishani, na kumalizia kusema kwamba Bale yuko levo za kina Ronaldo na Messi na anastahili kucheza ligi ya mabingwa Ulaya na kushinda mataji, na kuwa mchezaji bora wa dunia.
  No smiles: Bale, who could end up as the world's most expensive player, has a lot on his mind
  Hacheki mtu: Bale, ananafasi ya kuwa mchezaji ghali duniani, anawaza mengi hapa

  Hakuna shaka kwamba Madrid wako radhi kutoa kiasi cha pauni milioni 85 kwa ajili ya Bale, lakini Mwenyekiti Daniel Levy anataka kuona ofa pauni milioni 100.
  Licha ya tabia ya Bale kubadilika hawezi kufanya yale yaliyefanywa na Luka Modric kiangazi mwaka jana kwa kuondoka kwenye timu kulazimisha uhamisho wake Real.
  Na sasa hivi Madrid wanatamani Bale kufanya tabia kama zile za Modric.
  Uwepo wa Modric kwenye kikosi cha Madrid utamsaidia Bale kuzoea haraka mazingira mapya ya Bernabeu kama akihamia huko.
  Lakini kocha wa zamani wa England na Spurs, Glenn Hoddle anahisi kwamba Bale hayupo tayari kwenda kucheza nje ya England.
  Hoddle anaamini kila mchezaji anathamani yake, lakini anaamini itakuwa vizuri kwa Bale kuendelea kubaki Tottenham kwa sasa na kuendelea pale alipoishia kwenye msimu wa 2012-13.
  On his way: Bale held talks with Spurs chief Daniel Levy after a change of heart of his proposed move to Spain

  Huyooo: Bale amezungumza na Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy baada ya kubadili mawazo na kutaka kwenda Hispania
  Bale
  Crunch talks: Gareth Bale will discuss his future with agent Jonathan Barnett and Daniel Levy and the Tottenham chairman is likely to bow to the player's requests if the price is met by Real Madrid
  Mazungumzo: Bale (Juu) atazungumza kuhusu mustakabali wake na wakala Jonathan Barnett (picha ya chini kushoto) na Daniel Levy (kulia) na kuna kila dalili kwamba Levy atalazimika kukubali maombi ya Bale kama ofa ya maana zaidi itakuja.
  Join us: Zinedine Zidane (right), with Real boss Carlo Ancelotti, have been on a charm offensive
  Njoo: Zinedine Zidane (Kulia), akiwa na kocha wa Real, Carlo Ancelotti, wanaongoza mashambulizi ya kunasa Bale

  Hoddle, ambaye anajua inafananaje kuondoka Spurs na kutoka nje ya England, baada ya kuihama Spurs na kwenda Monaco mwaka 1987, aliongeza kusema kwamba ni kitu rahisi kuonyesha kiwango cha juu, lakini kubaki na kiwango hicho ndiyo kazi zaidi.
  Hoddle alisema “Hofu yangu ni kuwa amekuwa akipata tisa ya 10 katika kila mechi, baadhi ya mabao amefunga yamekuwa ya kuvutia sana, na ndio maana watu wako tayari kulipa fedha nyingi kwa ajili yake na mashabiki wa Real Madrid watakuwa wanaamini kuwa naye na Ronaldo  kwenye kikosi kimoja kunaipa timu nafasi ya kutoa upinzani Ulaya tena.
  “Unapoenda nje ya nchi miezi minne, mitano, sita ya mwanzo inakuwa migumu sana kufikia kiwango kile na kama familia yake itakuwa mbali atapata wakati mgumu zaid. Nahisi anaweza kuwa na msimu mbaya, kama anataka kwenda kucheza soka ni bora asubiri mwaka mmoja au miwili.”
  Touchline: Tottenham manager Andre Villas-Boas was desperate to keep hold of his key man
  Mstari wa kuingia uwanjani: Kocha Tottenham,  Andre Villas-Boas anahaha kumbakiza mchezaji wake muhimu
  World record: The deal for Bale eclipses the £80m fee Real paid for star man Cristiano Ronaldo in 2009
  Rekodi ya dunia: Dili ya kumnasa Bale itafunika dau la pauni milioni 80 ambalo Real walilipa kwa ajili ya Cristiano Ronaldo mwaka 2009 
  Holding his hands up: Bale will only consider moving to Real Madrid at this stage, not Manchester United
  Nainua mikono: Bale anawazo moja tu kwa sasa kwenda Real Madrid na siyo Manchester United 
  Bale
  Bale
  Njiani: vyombo vya habari vya Hispania vinaanza kutabiri ujio wake
  Poster boy: Bale is a valuable marketing tool for Spurs, with this poster in Times Square, New York
  Tangazo: Bale bidhaa adimu sokoni kwa Spurs, bango lake liko Times Square, New York
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BALE AAMUA KAMA NOMA NA IWE NOMA, AMUAMBIA VILLA BOAS USO KWA PUA; "NAONDOKA ZANGU" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top