• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 30, 2013

  SIMBA DAY YASOGEZWA MBELE, TP MAZEMBE NA SAMATTA WAOTA MBAWA

  Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 30, 2013 SAA 2:14 ASUBUHI
  TAMASHA la kuazimisha siku ya Simba SC linaweza kusogezwa mbele kwa simu mbili, kupisha sikukuu ya Eid El Fitri hivyo kufanyika Agosti 10, badala ya Agosti 8, kama ilivyo kawaida yake.
  Aidha, mpango wa Simba SC kucheza na mabingwa wa Afrika mara nne, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umeshindikana kutokana na timu hiyo ya Lubumbashi kutingwa na michuano ya Kombe la Shirikisho.
  Simba SC

  Na kwa sababu hiyo, timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam sasa itacheza na SC Villa ya Uganda katika tamasha hilo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Simba ilitumai kucheza na Mazembe yenye wachezaji wake wa zamani wawili, Mbwana Samatta na Patrick Ochan ambao iliwauzua klabu hiyo miaka miwili iliyopita, lakini ratiba ya michuano ya CAF imeharibu mambo. 
  Katika maendeleo mengine, wachezaji wa Simba SC waliokuwa na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanatarajiwa kujiunga na wenzao kambini, Bamba Beach, Kigamboni kuanzia leo jioni.
  Wachezaji waliokuwa Stars ni viungo Amri Kiemba na Haroun Chanongo. Kiemba alicheza dakika zote 90 na kufunga la Stars ikilala 3-1 Uwanja wa Mandela, Namboole na kutolewa jumla ya mabao 4-1, baada ya awali kufungwa 1-0 Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, wakati Chanongo aliingia uwanjani dakika ya 78 kumpokea John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC.     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA DAY YASOGEZWA MBELE, TP MAZEMBE NA SAMATTA WAOTA MBAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top