• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 26, 2013

  FABREGAS SASA AKAA MKAO WA KUELEKEA MAN UNITED

  IMEWEKWA JULAI 26, 2013 SAA 3:01 ASUBUHI
  KIUNGO Cesc Fabregas amewaambia rafiki zake England kwamba anataka kuondoka Barcelona kuhamia Manchester United.
  Kiungo huyo wa Hispania kwa sasa anagombewa na United na Barcelona, na mabingwa hao wa Ligi Kuu y England wamekwishatoa ofa ya Pauni Milioni 30.
  Kocha wa United, David Moyes aliwaambia Waandishi wa Habari nchini Japan jana kwamba mpango wa klabu hizo kufanya biashara ya nyota huyo wa zamani wa Arsenal unaendelea na ofa nyingine itatolewa.
  Uncertain future: Cesc Fabregas could leave Barcelona for Manchester United
  Mustakabali haueleweki: Cesc Fabregas anaweza kuondoka Barcelona kutua Manchester United

  Lakini habari kwamba Fabregas amewaambia rafiki zake England kwamba anataka kuondoka Nou Camp hatimaye zinaweza kuwapa faraja United.
  Inafahamika Fabregas anavutiwa na ahadi ya kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza United na yuko tayari kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Arsenal, mshambuliaji wa United, Robin van Persie.
  Fabregas pia anaamini anaweza kutwaa taji la England na United kuunganisha na lile moja aliloshinda Hispania la La Liga msimu uliopita. 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameshinda taji la FA na Ngao ya Jamii pekee katika kipindi chake cha kuichezea Arsenal.
  Barcelona wameendelea kutia kauzibe wakiiambia United kwamba, kiungo wao hawamuuzi."Vidic, Nani nad Antonio Valencia wote wanacheza nao. Wayne Rooney pia anakimbia na katika kiwango ambacho tunafikiri atakuwa fiti. Atapiga hatia wiki hii,".
  Lure: The prospect of linking up with Robin van Persie again is tempting Fabregas
  Muungano wawezakana: Uwezekano wa Robin van Persie kuungana na Fabregas tena wawezekana
  New-look United: David Moyes and Steve Round are now in charge at Old Trafford
  Muonekano mpya United: David Moyes na Steve Round sasa ni makocha Old Trafford
  Fond memories: Van Persie and Fabregas combined with success at Arsenal
  Watarudisha enzi: Van Persie na Fabregas walifanya kazi pamoja kwa mafanikio Arsenal
  Talented squad: Fabregas may also be tempted by the chance to win trophies in English football
  Kikosi cha vipaji: Fabregas pia anaweza kuvutiwa na hamu ya kushinda katika soka ya England

  Iwapo Fabregas ataamua kuomba kuondoka, mambo yanaweza kubadilika.
  United inatarajiwa kucheza mechi yake ya nne katika ziara yake ya kujiandaa na msimu, leo ikimenyana na Cerezo Osaka saa 5:00 asubuhi za Uingereza.
  Van Persie anatarajiwa kucheza sehemu kidogo baada ya kupata ahueni ya maumivu yake, wakati Moyes pia amesema kwamba Nahodha wake, Nemanja Vidic — ambaye pia amekuwa majeruhi ameanza kucheza soka ya ushindani nyumbani England.
  Moyes alisema: "Kunakuwa kuna mechi za mazoezi siku nyingine Carrington. 
  New kit: There have been many changes around United since the end of the season
  Jezi mpya: Kuna mabadiliko mengi United tangu mwishoni mwa msimu
  Bullet train: The United squad have been travelling through Japan in style
  Treni ya umeme: Kikosi cha United kimekuwa kikisafiri kwa staili ya aina yake Japan 
  Talented: Fabregas is among the finest midfielders in the world
  Cesc Fabregas stats

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: FABREGAS SASA AKAA MKAO WA KUELEKEA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top