• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 22, 2013

  TAIFA STARS YAFUATA TIKETI YA CHAN KAMPALA KESHOKUTWA

  Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JULAI 22, 2013 SAA 6:08 MCHANA
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaondoka Mwanza keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.
  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
  Bila Mwinyi na Shomary; Kikosi cha Stars, wachezaji Mwinyi Kazimoto (katikati waliochuchumaa) na Shomai Kapombe (wa kwanza) kulia hawatakuwepo.

  Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
  Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TAIFA STARS YAFUATA TIKETI YA CHAN KAMPALA KESHOKUTWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top