• HABARI MPYA

    Saturday, July 20, 2013

    SIMBA SC ILIVYOONYESHANA KAZI NA URA LEO TAIFA

    IMEWEKWA JULAI 20, 2013 SAA 2:47 USIKU
    Mshambuliaji wa Simba SC, Zahor Pazi akimtoka beki wa URA ya Uganda, Jonathan Mugabi katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. URA ilishinda 2-1.

    Zahor Pazi akijiandaa kumlamba chenga Jonathan Mugabi

    Ramadhan Singano 'Messi' akimtoka Lutimba Yayo 

    Betram Mombeki wa Simba SC akimiliki mpira mbele ya mabeki wa URA

    Betram Mombeki akipasua ngome ya URA

    Ramadhani Singano 'Messi' akidhibitiwa na Oscar Agaba wa URA

    Elkanah Nkugwa wa URA aliyelala kuupitia mpira miguuni mwa Marcel Biniventura wa Simba SC

    Kipa wa Simba SC, Abbel Dhaira (kushoto) akishangaana na mabeki wake, Samuel Ssenkoom na Nassor Masoud 'Chollo' baada ya URA kupata bao la pili

    Derick Walullya akimtoka beki mwenzake, Issa Rashid 'Baba Ubaya' wa Simba SC

    Adeyoum Saleh Ahmed akipasua katikati ya mabeki wa URA

    Elkanah Nkugwa wa URA akimdhibiti Marcel Boniventura wa Simba SC

    Jonathan Mugabi wa URA baada ya kuumizwa kwa kiwiko Betram Mombeki wa Simba SC hadi akashindwa kuendelea na mchezo. Mombeki alitolewa kwa kadi nyekundu.

    Ramadhan Singano 'Messi' akionyesha utundu wa kucheza na mpira hadi chini

    Raha ya mechi bao; Wachezaji wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba Ubaya' na Zahor Pazi wakimpongeza Betram Mombeki kwa kufunga bao

    Marcel Boniventura akikabiliana na Derick Walullya

    11 wa URA walioanza leo

    11 wa Simba SC walioanza leo

    Simba SC ya wazalendo; Kocha Mkuu wa Simba SC, Alhaj ABdallah Athumani Seif 'King  Kibaden' kushoto, akiwa na Msaidizi wake, Jamhuri Mussa Kihwelo na Meneja Nicodemus Menard Nyagawa kulia

    Nahodha wa URA, Joseph Owino akiwaongoza wachezaji wenzake wa timu hiyo ya Uganda kuwasalimia wachezaji wa Simba SC

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC ILIVYOONYESHANA KAZI NA URA LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top