• HABARI MPYA

    Tuesday, July 16, 2013

    CHELSEA ZA USO, CAVANI ATUA PARIS NA KUFANYIWA VIPIMO TAYARI KUTUA PSG

    IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 9:43 USIKU
    MSHAMBULIAJI Edinson Cavani yuko katika hatua za mwishoni za kutua Paris St Germain kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 55.
    Muuwaji huyo wa Uruguy atajiunga na klabu hiyo akitokea Napoli ya Italia baada ya kukataa kuhamia Ligi Kuu ya England.
    Manchester City na Chelsea zote zilikuwa zinataka kumsajili mchezaji huyo lakini ameamua kwenda Ufarasa.
    All smiles: Edinson Cavani leaves Pitie Salpetriere hospital in Paris after taking medical ahead of his move to PSG
    Wote wanatabasamu: Edinson Cavani akiondoka katika hospitali ya Pitie Salpetriere baada ya kufanyiwa vipimo kuelekea kujiunga na PSG
    Cavani alitua katika ardhi ya Paris Jumatatu na alionekana akiondoka katika hospitali ya Pitie Salpetriere baada ya kukamilisha vipimo. 
    Mabingwa hao wa Ufaransa watafanya Mkutano na Waandishi wa Habari Jumanne kwa ajili ya kumtambulisha mchezaji wao huyo mpya.
    Habari hizi zitakuwa pigo kubwa kwa timu za Ligi Kuu ya England.
    Star attraction: Cavani waves to the fans in France after completing his check-up
    Mvuto wa nyota: Cavani akiwapungia mashabiki nchini Ufaransa baada ya kukamilisha vipimo vya afya
    Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anataka kuongeza mshambuliaji na mustakabali wa Fernando Torres na Demba Ba upo shakani katika klabu hiyo.
    City, wakati huo huo, imewapoteza Carlos Tevez na Mario Balotelli katika miezi ya karibuni na kubaki na Sergio Aguero na Edin Dzeko katika safu ya ushambuliaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHELSEA ZA USO, CAVANI ATUA PARIS NA KUFANYIWA VIPIMO TAYARI KUTUA PSG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top