• HABARI MPYA

  Saturday, July 07, 2018

  MAREFA WATAKIWA KUJIGHARAMIA KUSHIRIKI KOZI ZA TFF KUJIANDAA KUCHEZESHA LIGI KUU MSIMU UJAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAREFA watakaoshiriki Kozi ya Utimamu wa mwili kwa ajili ya kuchezesha mechi za Ligi Kuu, Daraja la kwanza (FDL) na Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2018/2019 wametakiwa kujigharamia kwenda vituoni Mwanza na Dar es Salaam.
  Taarifa ya Ofisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo imesema kwamba kozi hiyo itahusisha waamuzi wote wa Daraja la Kwanza nchini, waliochezesha Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) na waliochezesha mashindano ya U20 ya Uhai Cup.
  "Kila Mwamuzi atatakiwa kujigharamia na ndio maana TFF imeweka vituo viwili ili kupunguza makali ya gharama. Kila Mwamuzi atatakiwa kuja na Passport size 2 kwaajili ya kuingia kwenye data za kiuamuzi na atatakiwa kujaza fomu ya taarifa binafsi,"imesema taarifa.

  Kituo cha Dar es Salaam kitakuwa na mikoa ya Dar es Salaam yenyewe,Pwani,Morogoro,Dodoma,Tanga,Iringa,Njombe,Mbeya,Ruvuma,Songwe,Lindi,Mtwara na Katavi.
  Kituo cha Mwanza kitakuwa na Mwanza yenyewe,Kagera,Geita, Mara, Simiu, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Rukwa.

  RATIBA YA KOZI
  Julai 13, 2018 Kuwasili
  Julai 14,2018 Usajili na kupima vituo vya Mwanza na Dar es Salaam
  Julai 15,2018 Utimamu na Semina (Asubuhi na Mchana)
  Julai 16,2018 Mtihani wa Waamuzi
  Julai 17,2018 Kuwasili Makamishna/Kujiorodhesha
  Julai 18,2018 Semina na Mtihani kwa Makamishna
  Julai 19,2018 Kusafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam
  Julai 21,2018 Kusahihisha Mtihani na kuteua Waamuzi/Makamishna
  Julai 23,2018 Kupanga ratiba za Ligi Kuu,FDL na SDL
  Julai 27,2018 Kukamilisha Upangaji wa ratiba
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAREFA WATAKIWA KUJIGHARAMIA KUSHIRIKI KOZI ZA TFF KUJIANDAA KUCHEZESHA LIGI KUU MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top