• HABARI MPYA

  Tuesday, April 02, 2024

  YANGA WAWASILI SALAMA AFRIKA KUSINI, WAMZAWADIA JEZI BALOZI BWANA


  RAIS wa Yanga SC, Hersi Ally Said (kulia) akimkabidhi jezi ya klabu hiyo Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana baada ya Mabingwa hao wa Tanzania kuwasili nchini humo kwa ajili ya mchezo na wenyeji, Mamelodi Sundowns Ijumaa.
  Yanga SC watamenyana na Mamelodi Sundowns katika mchezo wa marudiano wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria.
  Yanga inahitaji ushindi au sare ya mabao ili kwenda Nusu Fainali kufuatia sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAWASILI SALAMA AFRIKA KUSINI, WAMZAWADIA JEZI BALOZI BWANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top