• HABARI MPYA

  Tuesday, April 02, 2024

  KOCHA ALIYESHINDA MATAJI MFULULIZO SIMBA SC DK ADEL ZRANE AFARIKI DUNIA


  ALIYEWAHI kuwa Kocha wa Fitness (Utimamu wa Mwili) wa Simba SC, Mtunisia, Dk. Adel Zrane amefariki dunia leo Jijini Kigali nchini Rwanda ambako alikuwa mwajiriwa wa klabu ya APR.
  Kocha amefariki mapema leo asubuhi wakati anaondoka nyumbani kwenda mazoezini, ingawa sababu za kifo chake bado hazijajulika.
  Kufuatia msiba huo, APR ikaahirisha mazoezi ya asubuhi leo kujiandaa na mechi ya 26 ya msimu wa Ligi Kuu ya Rwanda.
  Dk. Adel Zrane amefariki akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi ka Rwanda ambao ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
  Zrane alijijengea heshima kubwa alipokuwa anafanya kazi kwa vigogo wa Tanzania, Simba SC ambako msimu wa mwaka 2018-19, akiwa kazini Msimbazi timu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Ngao ya Jamii chini ya Kocha Mkuu Mbelgiji, Patrick Aussems.
  Msimu uliofuata 2019-20, akiwa chini ya Mbelgiji mwingine, Sven Vandenbroeck wakashinda mataji yote matatu, Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Soka (TFF) na Ngao ya Jamii.
  Na pia msimu uliofuatia 2020-21, akiwa chini ya Mfaransa, Didier Gomez Da Rosa wakasomba tena mataji yote matatu, Ligi Kuu, TFF na Ngao, kabla ya kuondoka Msimbazi.
  Na ni katika kipindi hicho Simba SC ilikuwa na wachezaji wenye utimamu mkubwa kimwili na kuweza kufika Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Nara tatu mfululizo.
  Dk. Zrane amefundisha timu nyingine pia, He Etoile Sportif du Sahel ya kwao, Al Ain ya Saudi Arabia, Al-Wehdat Sportif Club ya Jordan na timu ya taifa ya Mauritania iliyoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2022.
  Mungu ampumzishe kwa amani Dk. Adel Zrane.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA ALIYESHINDA MATAJI MFULULIZO SIMBA SC DK ADEL ZRANE AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top