• HABARI MPYA

  Saturday, April 06, 2024

  SINGIDA BLACK STARS YAITANDIKA KMC 3-0 KOMBE LA TFF


  TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Singida Black Stars ambayo zamani ilikuwa inajulikana kama Ihefu SC yamefungwa na mshambuliaji Mkenya, Elvis Rupia dakika ya 13, kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya 16 na beki Andrew Vincent ‘Dante’ aliyejifunga dakika ya 23.
  Kwa matokeo hayo Black Stars inakuwa timu ya tano kutinga Robo Fainali Kombe la TFF baada ya Coastal Union, Namungo FC, Geita Gold na Tabora United.
  Coastal Unión iliitoa JKT Tanzania kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya bila kufungana Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Namungo FC iliitoa Kagera Sugar kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya bila kufungana Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Geita Gold iliitoa Rhino Rangers ya Tabora kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita na Tabora United iliitoa Singida Fountain Gate kwa kuichapa 3-0 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAITANDIKA KMC 3-0 KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top