• HABARI MPYA

  Saturday, April 06, 2024

  DE BRUYNE APIGA MBILI MAN CITY YAWACHAPA CRYSTAL PALACE 4-2


  KIUNGO Mbelgiji, Kevin De Bruyne amefunga mabao mawili kuiwezesha Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Venue Selhurst Park Jijini London.
  Kevin De Bruyne (32) amefunga mabao yake dakika ya 13 na 70, huku mabao mengine ya mabingwa hao watetezi yakifungwa na kinda wa miaka 19 wa England, Rico Lewis dakika ya 47 na mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland dakika ya 66.
  Kwa upande wao Crystal Palace mabao yao yamefungwa na washambuliaji Wafaransa, Jean-Philippe Mateta dakika ya tatu na Odsonne Édouard dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 70 katika mchezo wa 31 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na vinara Liverpool ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Crystal Palace wao baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 31 nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE BRUYNE APIGA MBILI MAN CITY YAWACHAPA CRYSTAL PALACE 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top