• HABARI MPYA

  Tuesday, April 02, 2024

  SIMBA SC YAIFUATA AL AHLY KESHO ALFAJIRI NA ‘FULL SQUAD’


  KIKOSI cha Simba SC kinatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kesho kwenda Cairo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Al Ahly Ijumaa.
  Simba wanakabiliwa na shinikizo la ushindi wa ugenini lazima dhidi ya Mabingwa hao watetezi, Al Ahly kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mechi ya kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa jumla katí ya Al Ahly na Simba atakwenda kumenyana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambazo mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.
  PICHA ZA MAZOEZI YA MWISHO SIMBA KABLA YA SAFARI
  VÍDEO: AFISA HABARI WA SIMBA AHMED ALLY AKIZUNGUMZIA SAFARI

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIFUATA AL AHLY KESHO ALFAJIRI NA ‘FULL SQUAD’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top