• HABARI MPYA

  Wednesday, April 03, 2024

  GEITA GOLD YATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE KA TFF KWA KUICHAPA RHINO RANGERS 2-1


  TIMU ya Geita Gold imefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora leo Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Yamlinga Yamlinga aliyejifunga dakika ya pili na Elius Maguri dakika ya 20, wakati bao pekee la Rhino Rangers limefungwa na Marky Simon.
  Geita Gold inakuwa timu ya pili kwenda Robó Fainali baada ya Namungo FC ambayo jana iliitoa Kagera Sugar kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya bila kufungana Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YATINGA ROBÓ FAINALI KOMBE KA TFF KWA KUICHAPA RHINO RANGERS 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top