• HABARI MPYA

  Thursday, April 04, 2024

  ARSENAL YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA LUTON TOWN 2-0


  TIMU ya Arsenal imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Luton Town usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Norway, 
  Martin Odegaard dakika ya 24 na beki Mjapan, Daiki Hashioka aliyejifunga dakika ya 44.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 68 katika mchezo wa 30 na kurejea kileleni, ikiizidi pointi moja Liverpool ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati mabingwa watetezi, Manchester City sasa wapo nafasi ya tatu kwa pointi zao 67 za mechi 30 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA LUTON TOWN 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top