• HABARI MPYA

  Friday, April 05, 2024

  COLE PALMER APIGA HAT TRICK CHELSEA YAICHAPA MAN UNITED 4-3


  WENYEJI, Chelsea FC wameibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Ulikuwa usiku mzuri kwa kiungo mshambuliaji kinda wa miaka 21, Muingereza Cole Jermaine Palmer aliyepiga hat trick kwa mabao yake ya dakika za 19 na 90'+10 yote kwa penalti na la dakika ya 90'+11 akimalizia pasi ya kiungo Muargentina Enzo Fernández.
  Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na kiungo mwingine Muingereza, Conor John Gallagher dakika ya nne, wakati mabao ya Manchester United yalifungwa na winga Muargentina Alejandro Garnacho Ferreyra dakika ya 34 na 67 na kiungo Mreno Bruno Fernandes dakika ya 39.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 29 na kusogea nafasi ya 10, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 48 za mechi 30 nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COLE PALMER APIGA HAT TRICK CHELSEA YAICHAPA MAN UNITED 4-3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top