• HABARI MPYA

  Friday, April 05, 2024

  LIVERPOOL YAREJEA KILELENI ENGLAND BAADA YA KUICHAPA SHEFFIELD UNITED 3-1


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na 
  Darwin Nunez dakika ya 17, Alexis Mac Allister dakika ya 76 na Cody Gakpo dakika ya 90, wakati bao pekee la Sheffield United alijifunga beki Conor Bradley dakika ya 58.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 70 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Arsenal wote wakiwa mbele ya mabingwa watetezi Manchester City wenye pointi 67 kufuatia wote kucheza mechi 30.
  Kwa upande wao Sheffield United baada ya kichapo hicho cha Anfield wanabaki na pointi zao 15 za mechi 30 pia mkiani mwa Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAREJEA KILELENI ENGLAND BAADA YA KUICHAPA SHEFFIELD UNITED 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top