• HABARI MPYA

  Tuesday, September 07, 2021

  MANARA APOKEWA VIZURI NA WAZEE YANGA

   AFISA mpya wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hajji Sunday Manara amepata mapokezi mazuri leo makao makuu ya klabu hiyo, Jangwani Jijini Dar es Salaam.
  Wazee wa klabu hiyo na wanachama kwa ujumla wamempokea kwa shangwe Manara ambaye amejiunga na klabj hiyo kutoka kwa mahasimu wa jadi, Simba.
  Akitoa shukrani zake kwa mapokezi hayo, Manara amesema; “Ndugu zangu katika siku ngumu ni ambayo unapokewa na watu ambao wewe unastahili kuwapokea, kwa mila na desturi zetu Afrika, wazee wanapokewa na vijana, lakini kwa umaalum mlionifanyia leo ni deni zito, sijawai kupata mapokezi mazito kutoka kwa wazee wangu kama siku ya leo, deni hili pia ninalo kwa Wanachama wote wa Yanga nchi nzima,".


  Manara ameomba radhi kwa kwenda kufanya kazi Simba wakati baba yake mzazi, Sunday Ramadhani Manara ni mchezaji wa zamani wa Yanga na mwanachama pia naye akizaliwa wakati baba yake anacheza Jangwani miaka ya 1970.
  Manara amesema hata yeye amecheza timu ya vijana ya Yanga chini ya kocha marehemu Tarzany Kessy na akasikitika mno kuhamia upande wa pili.
  Mbali na baba yake mzazi kucheza Yanga, baba yake mkubwa Kitwana na baba yake mdogo, Kassim pia wamecheza Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANARA APOKEWA VIZURI NA WAZEE YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top