• HABARI MPYA

  Monday, September 06, 2021

  AZAM FC WAREJEA DAR KUWASUBIRI WASOMALI

  KIKOSI cha Azam FC kimerejea nchini jana baada ya kambi ya wiki moja na ushei Jijini Ndola Ndola nchini Zambia kujiandaa na msimu mpya tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.
  Azam FC watakuwa wenyeji wa Horseed ya Somalia Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 18 Uwanja wa Garoonka Banadir Jijini Mogadishu.
  Ikiwa Zambia, Azam FC ilipata mechi tatu za kujipima nguvu – ikishinda mbili zote 1-0 dhidi ya Zesco, bao pekee la kiungo Mzambia, Rodgers Kola na Kabwe Worries bao la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo baada ya kuchapwa 4-0 na Red Arrows zote Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.


  Pamoja na hayo, Azam FC ilisajili beki mpya wa kati wa Azam FC, Mcameroon, Yvan Lionnel Mballa kwa mkataba wa mwaka mmoja kutoka Forest Rangers ya Zambia.
  Huyo amekuwa mchezaji mpya wa nane Azam baada ya viungo, Mkenya Kenneth Muguna, Wazambia Paul Katema, Charles Zulu na washambuliaji Rodgers Kola na Mkongo Idris Mbombo na wazawa, kipa Ahmed Ali Suleiman 'Salula' kutoka KMKM ya Zanzibar na beki, Edward Charles Manyama kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAREJEA DAR KUWASUBIRI WASOMALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top