• HABARI MPYA

  Monday, September 06, 2021

  MECHI YA BRAZIL NA ARGENTINA YAVUNJIKA

  MECHI ya kufuzu Kombe la Dunia kwa Amerika Kusini baina ya wapinzani wakubwa, Brazil na Argentina ilivunjika jana baada ya dakika saba tu Jijini Sao Paulo kufuatia wachezaji watatu wa Argentina wanaocheza England kukiuka taratibu za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
  Hao ni kipa Emiliano Martínez na winga Emiliano Buendía wa Aston Villa, beki wa kati Cristian Romero na kiungo Giovani Lo Celso wa Tottenham Hotspur na sasa mchezo utapangiwa siku nyingine.
  Brazil inaongoza mbio za kwenda Qatar mwakani kwa Amerika Kusini ikiwa na pointi 21, sita zaidi ya Argentina yenye poijnti 15 baada ya mechi saba.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA BRAZIL NA ARGENTINA YAVUNJIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top