• HABARI MPYA

  Tuesday, March 26, 2019

  UFARANSA YAICHAPA 4-0 ICELAND KUFUZU EURO 2020

  Kikosi cha Ufaransa kabla ya mchezo wa Kundi H kufuzu Euro 2020 dhidi ya Iceland usiku wa jana Uwanja wa Stade de France mjini Paris. Ufaransa ilishinda 4-0, mabao yake yakifungwa na Samuel Umtiti dakika ya 12, Olivier Giroud dakika ya 68, Kylian Mbappe dakika ya 78 na Antoinne Griezmann dakika ya 84. Uturuki nayo iliichapa 4-0 Moldova mjini Eskisehir katika mchezo mwingine wa kundi hilo na sasa ina pointi sita sawa na Ufaransa, wakifuatiwa na Albania na Iceland zenye pointi tatu kila moja 
    

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UFARANSA YAICHAPA 4-0 ICELAND KUFUZU EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top