• HABARI MPYA

  Monday, March 18, 2019

  LIVERPOOL YASHINDA 2-1 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND

  Mtokea benchi, James Milner (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Liverpool bao la ushindi kwa penalti dakika ya 81 ikiilaza 2-1 Fulham Uwanja wa Craven Cottage mjini London katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na kurejea kileleni, ikifikisha pointi 76 katika mchezo wa 31, sasa ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.
  Bao la kwanza la Liverpool lilifungwa na Sadio Mane dakika ya 26 akimalizia pasi ya Roberto Firmino, kabla ya Ryan Babel kuisawazishia Fulham dakika ya 74 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YASHINDA 2-1 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top