Mkongwe Fabio Quagliarella akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Italia dakika za 35 na 45 na ushei yote kwa penalti katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Liechtenstein kwenye mchezo wa Kundi J kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Ennio Tardini mjini Parma. Mabao mengine ya Italia yalifungwa na Stefano Sensi dakika ya 17, Marco Verratti dakika ya 32, Moise Kean dakika ya 69 na Leonardo Pavoletti dakika ya 76 na kwa ushindi huo The Azzurri inafikisha pointi sita kufuatia kushinda mechi zake zote mbili za mwanzo ikifuatiwa na Ugiriki yenye pointi nne. Mechi nyingine za kundi hilo jana Bosnia-Herzegovina ililazimishwa sare ya 2-2 Ugiriki mjini Zenica na Finland ikawachapa wenyeji, Armenia 2-0 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Nigerian fans drive SuperSport’s 19.1bn World Cup Digital Views
-
Nigerian football fans were among the biggest participants in SuperSport’s
digital FIFA World Cup 2026 experience, accounting for 21.2 percent of
users o...
49 seconds ago



.png)
0 comments:
Post a Comment