• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2019

  MBIO ZA AFCON 2019 ZAKAMILISHWA, AFRIKA MASHARIKI YANG'ARA

  MBIO za kuwania tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 zimekamilishwa jana huku timu nne za Afrika Mashariki, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania zikifuzu.
  Fainali za AFCON mwaka huu zitafanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 nchini Misri na hiyo ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwapokonya uenyeji Cameroon.
  Kutoka kundi A zilizofuzu ni Senegal na Madagascar zilizozipiku Equatorial Guinea na Sudan, kutoka Kundi B Morocco na Cameroon zilizozipiku Malawi na Comoro, kutoka Kundi C Mali na Burundi zilizozipiku Gabon na Sudan Kusini, kutoka Kundi D Algeria na Benin zilizozipiku Gambia na Togo na Kundi E ni Nigeria na Afrika Kusini zilizozipiku Libya na Shelisheli.
  Nyingine ni kutoka Kundi F ambazo ni Ghana na Kenya zilizozipiku Ethiopia na Sierra Leone, kutoka Kundi G Zimbabwe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zilizozipiku Liberia na Kongo, kutoka Kundi H ni Guinea na Ivory Coast zilizozipiku Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Rwanda.
  Nyingine ni kutoka kutoka Kundi I Angola na Mauritania zilizozipiku Burkina Faso na Botswana, kutoka Kundi J Tunisia na Misri zilizozipiku Niger na Eswatini, kutoka Kundi K Guinea-Bissau na Namibia zilizozipiku Msumbiji na Zambia na kutoka Kundi L Uganda na Tanzania zilizopiku Lesotho na Cape Verde.
  Droo ya kupanga makundi ya AFCON ya mwaka huu ambayo kwa mara ya kwanza itashirikisha timu 24 kutoka 16, itafanyika 12 Aprili 12 mjini Cairo nchini Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBIO ZA AFCON 2019 ZAKAMILISHWA, AFRIKA MASHARIKI YANG'ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top