• HABARI MPYA

  Wednesday, March 27, 2019

  GARDIEL MICHAEL ATIMKIA NCHINI AFRIKA KUSINI KUFANYA MAJARIBIO SUPERSPORT UNITED

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kushoto wa Yanga SC, Gardiel Michael Mbaga ameondoka leo mjini Dar es Salaam kwenda kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini.
  Gardiel alikuwepo kwenye kikosi cha Tanzania kilichoifunga Uganda mabao 3-0 Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu.
  Na mchezaji huyo wa zamani wa Azam FC ndiye aliyeseti bao la kwanza la Taifa Stars lililofungwa na winga wa zamani wa Yanga, Simon Happygod Msuva ambaye kwa sasa anachezea Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco.

  Gardiel Michael amekwenda kufanya majaribio klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini 

  Na baada ya kazi nzuri kuisaidia nchi yake kurejea AFCON baada ya miaka 39, tangu ishiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza 1980, Gardiel anakwenda kujaribu kucheza soka ya kulipwa nje ya Tanzania.
  Mchezaji huyo mzaliwa wa Tanga ameondoka kwa baraka za uongozi wa klabu yake na atakuwa huko kwa wiki moja akifanya majaribio.
  Maana yake Mbaga atakosekana kwenye mchezo wa Jumamosi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Alliance FC mjini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GARDIEL MICHAEL ATIMKIA NCHINI AFRIKA KUSINI KUFANYA MAJARIBIO SUPERSPORT UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top