• HABARI MPYA

  Sunday, March 17, 2019

  HII NDIYO SIMBA SC ILIIPIGA YANGA 4-1 PALE TAIFA JULAI 2 MWAKA 1994

  Kikosi cha Simba SC kabla ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi Kuu) Tanzania Bara Julai 2, mwaka 1994 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam. Kutoka kulia waliosimama George Masatu, Mustapha Hoza, Hussein Marsha, Mwameja Mohammed, Godwin Aswile, Madaraka Suleiman na Mfadhili, Azim Dewji. Waliochuchumaa kutoka kulia Edward Chumila (marehemu), Iddi Suleiman ‘Meya’, Deo Mkuki, Duwa Said na Athumani China. Simba SC ilishinda 4-1 mabao yake yakifungwa na George Masatu, Athumani China, Madaraka Selemani na Dua Saidi wakati bao pekee la Yanga SC lilifungwa na Constantine Kimanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HII NDIYO SIMBA SC ILIIPIGA YANGA 4-1 PALE TAIFA JULAI 2 MWAKA 1994 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top