• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 16, 2019

  TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI KESHO BAHARI BEACH MAANDALIZI MECHI NA UGANDA MACHI 24

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinatarajiwa kuingia kambini kesho katika hoteli ya Bahari Beach iliyopo Kunduchi mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baadaye mwezi huu.
  Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Uganda, The Cranes Machi 24, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa Kundi L kufuzu AFCON Juni 2019 nchini Misri.
  Na baada ya kikao cha pili cha Kamati ya Saidia Taifa Stars wiki hii mjini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kikosi kinaingia kambini kesho.

  Taifa Stars inahitaji ushindi tu katika mchezo huo wa mwisho ili kufuzu AFCON ya pili kihistoria, huku ikiombea matokeo mabaya Lesotho mbele ya Cape Verde mjini Praia katika mchezo mwingine wa mwisho wa Kundi L.
  Uganda tayari imejihakikishia kucheza AFCON ya Juni nchini Misri baada ya kufikisha pointi 13, wakati Lesotho inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake tano sawa na Tanzania na Cape Verde yenye pointi nne zote zina nafasi ya kuungana na The Cranes.
  Timu mbili zinatakiwa kufuzu kutoka kundi hilo na kama Lesotho itaifunga Cape Verde basi hata Taifa Stars ikiifunga Uganda haitafuzu kwa sababu katika mechi mbili dhidi ya Mamba ilitoa sare na kufungwa ugenini. 
  Pamoja na kwamba imekwishafuzu, lakini Uganda inayofundishwa na Mfaransa, Sebastien Desabre imepania kutopoteza mechi hiyo na imepanga kuweka kambi yake mjini Ismailia nchini Misri kuanzia kesho hadi Machi 22.
  Kikosi cha Taifa Stars kinachotarajiwa kuingia kambini kesho kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Aaron Kalambo (Tanzania Prisons), Metacha Mnata (Mbao FC) na Suleiman Salula (Malindi SC).
  Mabeki; Hassan Kessy (Nkana FC - Zambia), Gardiel Michael (Yanga SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Vincent Philipo (Mbao FC), Ally Mtoni ‘Sonso’ (Lipuli FC), Andrew Vincent ‘Dante’ (Yanga SC), Kennedy Wilson (Singida United) na Aggrey Morris (Azam FC).
  Viungo;  Feisal Salum (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba SC), Himid Mao (Petrojet FC - Misri), Mudathir Yahya (Azam FC), Shiza Kichuya (ENPPI - Misri), Simon Msuva (Difaa El Jadida – Morocco) na Farid Mussa (Tenerife B).
  Washambuliaji; Yahya Zayd (Ismailia - Misri), Shaaban Iddi Chilunda (CD Izara – Hispania), Rashid Mandawa (BDF XI - Botswana), Thomas Ulimwengu (JS Saoura - Algeria), John Bocco (Simba SC) na Mbwana Samatta (KRC Genk – Ubelgiji). 
  Naye ameita kikosi imara ambacho kinaundwa na  makipa; Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Jamal Salim (El Merreikh), Charles Lukwago (KCCA FC) na Nicholas Sebwato (Onduparaka FC).
  Mabeki; Isaac Isinde (Kirinya Jinja SS), Murushid Juuko (Simba SC), Timothy Awanyi (KCCA FC), Denis Iguma (Kazma FC), Nicholas Wadada (Azam FC), Musitafa Mujuzi (Proline FC), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia) FC, Isaac Muleme (Haras El Hodood), Joseph Ochaya (Lusaka Dynamo), Hassan Wasswa (El Geish), Khalid Aucho(Huru), Ibrahim Saddam Juma (KCCA FC), Tadeo Lwanga (Vipers SC), Opondo Moses( Vendsyssel) na Allan Kateregga (Cape Town City).
  Washambuliaji ni Faruku Miya (Gorica ), Moses Waisswa (Vipers Sc), Yunus Sentamu (FK Tirana), Martin Kizza (Sc Villa Jogoo), Allan Kyambadde (KCCA FC), Emmanuel Okwi (Simba SC), Edrisa Lubega (SV Ried), Derrick Nsibambi (Smouha), Patrick Kaddu (KCCA FC), William Luwagga Kizito (FC Bate Borisov) na Yasser Mugerwa (Fasil Kenema).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI KESHO BAHARI BEACH MAANDALIZI MECHI NA UGANDA MACHI 24 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top