• HABARI MPYA

  Sunday, March 24, 2019

  MWAKINYO AMTWANGA MUARGENTINA KO RAUNDI YA TANO NA KUTETEA TAJI LAKE

  Na Mwandishi Wetu, NAIROBI
  BONDIA Hassan Mwakinyo usiku wa jana amemshinda kwa Knockout (KO) raundi ya tano Sergio Eduardo Gonzalez wa Argentina katika pambano lililofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) mjini Nairobi nchini Kenya.
  Mwakinyo, kijana kutoka mkoani Tanga alimkalisha mpinzani wake huyo kutoka Amerika Kusini katika raundi ya tano katika pambano hilo la uzito wa Super Welter ambalo lilipangwa kufanyika kwa raundi tatu zaidi.
  Hilo linakuwa pambano la tano mfululizo Mwakinyo anashinda tangu Machi 10 mwaka 2018 alipomshinda Ambokile Chusa kwa pointi mjini Dar es Salaam, kabla ya kwenda kumpiga Muingereza Sam Eggington Septemba 8, 2018 mjini Birmingham, Said Yazidu Oktoba 20, 2018 na Joseph Sinkala Oktoba 28 2018 mjini Tanga, yote kwa KO.
  Hassan Mwakinyo jana amemshinda kwa KO raundi ya tano Sergio Gonzalez wa Argentina mjini Nairobi nchini Kenya.   Hassan Mwakinyo akimuadhibu Sergio Gonzalez katika pambano la jana mjini Nairobi  

  Kwa ujumla, Mwakinyo amepoteza mapambano mawili tu kati ya yote 17 aliyocheza akipigwa na Shaaban Kaoneka Mei 14 mwaka 2016 mjini Dar es Salaam na Mrusi Lendrush Akopian mjini Moscow Desemba 2 mwaka 2017.
  Baada ya ushindi huo, Mwakinyo ambaye ni bingwa wa taji la Kimataifa la UBO (Universal Boxing Organization) sasa anataka kuwania ubingwa wa dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAKINYO AMTWANGA MUARGENTINA KO RAUNDI YA TANO NA KUTETEA TAJI LAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top