• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 23, 2019

  BURUNDI YAWEKA HISTORIA, YAFUZU AFCON KWA MARA YA KWANZA

  BURUNDI imeandika historia baada ya kufuzu kwa mara ya kwanza kabisa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Juni mwaka huu chini hiyo.
  Hiyo ni baada ya Int’hamba Murugamba kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Gabon katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi C uliopigwa jioni ya leo Uwanja wa Prince Louis Rwagasore mjini Bujumbura.
  Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Cedric Amissi alianza kuifungia Burundi dakika ya 76, kabla ya Omar Ngando kujifunga kuisawazishia Gabon dakika ya 82.
  Matokeo hayo yanaifanya Burundi imalize na pointi 10 kwenye Kundi C, nyuma ya Mali walioongoza na ambao tayari wamekwishafuzu, huku Gabon wakimaliza na pointi nane katika nafasi tatu na Sudan Kusini wakishika mkia kutokana na kufungwa mechi zote.
  Burundi inakuwa taifa la tatu kutoka Afrika Mashariki kufuzu fainali hizo zitakazopigwa mwezi Juni mwaka huu nchini Misri, baada ya Uganda na Kenya.
  Kesho Tanzania ijaribu kuwa nchi ya nne ya ukanda wa CECAFA kufuzu AFCON ya mwaka huu itakapomenyana na Uganda Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam ikihitaji ushindi na huku ikiomba Lesotho itoe sare au kufungwa na Cape Verde mjini Praia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BURUNDI YAWEKA HISTORIA, YAFUZU AFCON KWA MARA YA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top