• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2019

  UJERUMANI YAICHAPA UHOLANZI 3-2 AMSTERDAM KUFUZU EURO 2020

  Nico Schulz akishangilia baada ya kuifungia Ujerumani bao la ushindi dakika ya 90 ikiwalaza wenyeji, Uholanzi 3-2 katika mchezo wa Kundi C kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Johan Cruijff Arena mjini Amsterdam. Ujerumani ilitangulia kwa mabao ya Leroy Sane dakika ya 25 na Serge Gnabry dakika ya 34, kabla ya Uholanzi kusawazisha kupitia kwa Matthijs De Ligt dakika ya 48 na Memphis Depay dakika ya 63. Mechi nyingine ya kundi hilo jana, Ireland Kaskazini iliichapa Belarus 2-1 na sasa inaongoza kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Uholanzi pointi tatu sawa na Ujerumani 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UJERUMANI YAICHAPA UHOLANZI 3-2 AMSTERDAM KUFUZU EURO 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top