• HABARI MPYA

  Tuesday, March 26, 2019

  ENGLAND YAENDELEZA UBABE KUFUZU EURO 2020, YASHINDA 5-1

  Raheem Sterling akifurahia baada ya kufunga bao la tano dakika ya 80 katika ushindi wa 5-1 wa England dhidi ya Montenegro kwenye mchezo wa Kundi A kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica. Mabao mengine ya England yalifungwa na Michael Keane dakika ya 30, Ross Barkley mawili dakika za 38 na 59 na Harry Kane dakika ya 71, wakati bao pekee la Montenegro limefungwa na Marko Vesovic dakika ya 17. Mechi nyingine ya Kundi A, Kosovo imelazimishwa sare ya 1-1 na Bulgaria mjini Pristina na sasa England inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita baada ya kushinda mechi zote mbili ikifuatia na Bulgaria yenye pointi mbili 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ENGLAND YAENDELEZA UBABE KUFUZU EURO 2020, YASHINDA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top