• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 12, 2019

  MTIBWA SUGAR YAITANDIKA SINGIDA UNITED 1-0 MANUNGU MECHI YA LIGI KUU BARA LEO

  Na Mwandishi Wetu, MANUNGU
  TIMU ya Mtibwa Sugar FC leo imeutumia vyema Uwanja wa nyumbani wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Ismail Aidan Mhesa dakika ya 25 na kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha Zubery Katwila inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda hadi nafasi ya tano kutoka ya nne.
  Singida United inayofundishwa na kocha Mserbia, Dragan Popadic baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi zake 33 ikifikisha mechi 29 za kucheza, ingawa inabaki nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu ya timu 20.

  Yanga SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 67, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 56 baada ya wote kucheza mechi 27, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 51 za mechi 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAITANDIKA SINGIDA UNITED 1-0 MANUNGU MECHI YA LIGI KUU BARA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top