• HABARI MPYA

  Tuesday, March 19, 2019

  SIMBA SC YAENDELEZA FURAHA KWA MASHABIKI WAKE, YAWAPIGA RUVU SHOOTING 2-0 TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imeendeleza furaha kwa mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ifikishe pointi 54 baada ya kucheza mechi 21, sasa ikizidiwa pointi tano na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake 59 za mechi 28, nyuma ya Yanga SC yenye pointi 67 za mechi 28.  
  Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Flerentina Zabron, Simba SC ilifunguka kipindi cha pili na kupata mabao yake yote mawili.

  Kabla ya mchezo wake, Maddie Kagere alikabidhiwa tuzo yake ya kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu mwezi Februari

  Alianza beki wa kati, Paul Bukaba Bundala kufunga la kwanza dakika ya 52 akimalizia shuti la kiungo Said Hamisi Ndemla baada ya mpira uliookolewa kufuatia krosi ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima aliyeanazishwa kona fupi na beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
  Akafuatia Meddie Kagere kufunga kwa penalti dakika ya 55 baada ya beki Tumba Lui Swedi wa Ruvu Shooting kumuangusha Adam Salamba kwenye boksi.
  Simba SC ingeweza kuvuna mabao zaidi kama ingetumia vyema nafasi zaidi ilizotengeneza kipindi cha pili. 
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Paul Bukaba, Yusuph Mlipili, Jonas Mkude, Rashid Juma/Haruna Niyonzima dk43, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Muzamil Yassin dk73, Adam Salamba na Hassan Dilunga/Meddie Kagere dk43.
  Ruvu Shooting; Abdallah Rashid, George Amani, Edward Manyama, Tumba Swedi, Santos Mazengo, Baraka Mtuwi, Shaaban Msala, Emmanuel Martin, William Patrick, Fully Maganga/Issa Kanduru dk84 na Hamisi Ismail/Said Dilunga dk60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEZA FURAHA KWA MASHABIKI WAKE, YAWAPIGA RUVU SHOOTING 2-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top