• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 15, 2019

  BASATA YARIDHIA MABADILIKO YA MFUMO WA UENDESHWAJI MISS TOURISM TANZANIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BARAZA la Sanaa  la Taifa (BASATA) limeridhia mabadiliko ya mfumo wa uongozaji wa shindano la Miss Utalii Tanzania, na kuluhusu kuendelea kutanyika nchini Tanzania mwaka huu 2019.
  Chini ya Mabadiliko hayo, shindano la Miss Utalii Tanzania sasa limeimarisha na kuborehsa mfumo wa uongozi kwa kuwa na mfumo rasmi wa uongozi na managementi “ Organisation structre”,na mfumo rasmi wa mashindano “Pageant Structure” katika ngazi zote. Mabadiliko hayo sasa yanalifanya shindano hilo kuwa kama yalivyomengine ya kimataifa kuendeshwa kwa mfumo wa ktaasisi yani Miss Tourism at an Institution Level”
  Chini ya mabadiliko hayo shindano la Miss Utalii Tanzania ,sasa litajulikana kama shindanola kimataifa la Miss Utalii Tanzania yani Miss Tourism Tanzania International Pageant. Hivyo kuandika historia ya kuwa miongoni mwa mashindano ya kimataifa ya utalii Duniani,na la kwanza na pekee la kimataifa Tanzania na Afrika mashariki na kati. Shindano hili sasa litakuwa na washiriki wa ndani (watanzania) wakiwakilisha mikoa na kanda zao ,na washiriki wanje (wasio watanzania) waki wakilisha  nchi zao katika fainali kimataifa za Taifa za Miss Tourism Tanzania International Pageant, kila mwaka,waki wania taji la Miss Utalii Tanzania na la Miss Tourism Tanzania International kila mwaka. Fainali ambazo zitarushwa mbashara (LIVE) duniani kote kutokea Tanzania ,kupitia Televisheni na mitandao ya kijamii, huku fainali hizo zikishudiwa na watazamaji zaidi ya 922 milioni duniani kote.
  Chini ya Mabadiliko ya mfumo wa uongozi na manejimenti mamlaka ya juu ya uongozi itakuwa ni  Advisory/Governing Board na kamati zake za utendaji ,huku mamlaka ya juu ya utendaji na manejimenti itakuwa ni Executive Board na idara zakeza utendaji na bodiza mshindanokatika kila ngazi. Hii ni hatua kubwakitaifaya mapinduzi ya sanaa ya urembo na mitindo nchini , na fulsa kwa jamii na taifa kutumia washiriki wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali duniani kujitangaza kitaifa na kimataifa, tofauti na mfumo wa awali ambapowashiriki kutoka nchini walikuwa wakitumika kutangaza nchi nyingine kwa kushiriki mashindano yanayo fanyika katika nchi hizo.
  Tofauti na mashindaono mengine ya urembo na mitindo  nchini ,ni shindano la Kimataifa la Miss Utalii Tanzania pekee ambalo washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani watakuja nchini kushiriki mashindano. Mabadiliko hayo pia yamegua na kuhusisha sifa za washiriki kwa kuziboresha na kuzifanya ziendane na matakwa ya mashindano ya kimataifa, sifa hizo za washiriki nipamoja na washiriki kuwa na cheti cha kuhitimu kidato cha sita au chuo au zaidi,mshiriki kuwa raia wa nchi anayo wakilisha,urefu wa angalau sentimeta 168 au zaidi,uwezo wa kuzumza lugha ya Taifa ya nchi anayo wakilisha , kutokuwahi kuolewa,au kujifungua,kuwa na jinsia ya kike kwa asili,wenye rangi asilia, utimamu wa afya  ya ,Akili,Viungo  na mwili, wenye malengo mahususi ya kuitumikia  jamii na  taifa, msukumo nafsi wa kushiriki mashindano na kutaka kushinda taji (Platform). 
  Malengo ya shindano hili pia  yameborehwa  ili  kukidhi matakwa  ya kuwa shindano la kimataifa, bila kuathili tamaduni na mila njema  za Tanzania na Afrika. Malengo mahususi ya mashindano haya ni kuunga mkono juhudi za serikali na mamlaka zake ,kwa kutafsiri kwa vitendo sera za Taifa  za Utalii, Utamaduni, Michezo, Wanyama pori, Misitu, Uwekezaji, Mazingira, Biashara, Viwanda,wanawake , Jinsia  na Watoto kitaifa na kimataifa. Ni malengo ya mashindano haya pia nikutangaza utalii ,utamaduni,na mianya ya uwekezaji ya Tanzania Kitifa na kimataifa. Pia ni malengo ya mashindano  haya kuhamasisha  na kukuza  utalii  wa ndani,Utalii wa Kitamaduni. Utalii wa michezo, Utalii wa Mikutano na vita dhidi ya Uwindaji Haramu, Uvuvi Haramu Uharibifu wa Mazingira, Umasikini, Ujinga, Maradhi,Tamaduni kongwe na potofu.  Kipekee ni malengo ya shindano hili kukuza na kuamasisha  uzalendo  na kujivunia  na kuthamini utaifa na maliasili  za Taifa bidhaa   za Tanzania  na kuhamasisha  matumizi ya Bidhaa  za Tanzania.  
  Mashindano ya kimataifa ya Miss Utalii Tanzania (Miss Tourism Tanzania International Pageant), yanaratibiwa na asasi ya Africa Tourism Promotion Center na Miss Tourism  Tanzania Organisation.Kalenda ya kudumu ya mashindano haya itatangazwa katika mkutano wa kimataifa na waandishi wa habari wa kitaifa na kimataifa ,utakao fanyika hivi karibuni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BASATA YARIDHIA MABADILIKO YA MFUMO WA UENDESHWAJI MISS TOURISM TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top