• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 11, 2019

  ZIDANE AREJESHWA KUWA KOCHA WA REAL MADRID HADI 2022

  KLABU ya Real Madrid imethibitisha kumteua tena Zinedine Zidane kuwa kocha wake Mkuu hadi mwaka 2022.
  Zidane amerejea kwenye klabu yake hiyo ghafla, kiasi cha miezi tisa tangu aondoke kufuatia kutwaa taji la tatu mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Klabu hiyo imejikuta katika wakati mgumu kutokana na matokeo mabaya chini ya kocha Santiago Solari hususan baada ya kutolewa na Ajax katika Ligi ya Mabingwa kwa kufungwa Uwanja wa Bernabeu.

  Zinedine Zidane amerejea kuwa kocha Mkuu wa Real Madrid hadi mwaka 2022 


  MATAJI ALIYOTWAA ZIDANE BERNABEU 

  La Liga: 2016–17
  Super cup ya Hispania: 2017 
  Ligi ya Mabingwa Ulaya: 2015–16, 2016–17, 2017–18 
  Super Cup ya UEFA: 2016, 2017 
  Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2016, 2017 
  Mataji yote haya alishinda Zinedine Zidane alipokuwa kocha wa Real Madrid awali
  Zidane aliiwezesha klabu hiyo ya Hispania kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kujiuzulu Mei mwaka jana.
  Kocha aliyechukua nafasi yake, Julen Lopetegui alifukuzwa mwezi Oktoba tu wakati huyu wa sasa Solari anaondolewa baada ya miezi minne tu kazini.
  Rais wa klabu, Florentino Perez alimuomba Zidane arejee baada ya Madrid kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Ajax, lakini ilionekana ni vigumu Mfaramsa huyo kurejea.
  Na hiyo kutokana wasiwasi wa namna ambavyo klabu imeyumba msimu huu baada ya kumuuza Cristiano Ronaldo msimu uliopita.
  Zidane alimkatalia Rais wake huyo wa zamani na ikaonekana kama Perez angemfuata Jose Mourinho.
  Perez alikuwa tayari kuweka mezani ofa ya Pauni Milioni 14.5 kwa Mourinho na inaelezwa ni kiasi hicho hicho cha ofa amepewa Zidane hadi akashawishika kurejea.
  Zidane alifanya kazi nzuri ya kukumbukwa katika timu hiyo ya mji mkuu wa Hispania, akishinda mataji tisa ndani ya miaka miwili na nusu kazini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZIDANE AREJESHWA KUWA KOCHA WA REAL MADRID HADI 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top