• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 15, 2019

  ARSENAL YAPEWA NAPOLI ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

  Arsenal itamenyana na Napoli, Chelsea na Slavia Prague katika Robo Fainali ya Europa League


   
  ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

  Napoli vs Arsenal
  Villarreal vs Valencia
  Benfica vs Frankfurt
  Slavia Prague vs Chelsea
  Mechi za kwanza zitachezwa Aprili 11 na marudiano Aprili 18.
  NUSU FAINALI 
  Napoli/Arsenal vs Villarreal/Valencia
  Benfica/Frankfurt vs Slavia Prague/Chelsea
  TIMU ya Arsenal ya England itamenyana na Napoli katika Robo Fainali ya Europa League. 
  Katika droo iliyopangwa leo mjini Nyon, Uswisi, kikosi cha Maurizio Sarri, Chelsea ambayo haijapoteza mechi hadi sasa kwenye mashindano haya, yenyewe itamenyana na Slavia Prague.
  Kutakuwa na mtanange wa timu za Hispania tupu kati ya Villarreal na Valencia wakati Benfica itamenyana na Frankfurt katika kuwania Nusu Fainali. Mechi za kwanza zitachezwa Aprili 11 na marudiano Aprili 18.
  Chelsea itaanzia nyumbani kwa sababu zote, The Blues na Arsenal haziwezi kucheza London katika usiku mmoja. 
  Mshindi wa mechi kati ya Chelsea na Slavia Prague atakutana na mshindi wa mechi kati ya Frankfurt na Benfica. 
  Arsenal wameshinda nyumbani tu katika mechi zao zilizopita dhidi ya Napoli kwenye michuano ya Ulaya, wakati walipowafunga wababe hao wa Serie A 2-0 kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2013-14, Mesut Ozil akihusika katika mabao yote.
  Mjerumani huyo alifunga na kutoa pasi ya bao lingine kwenye mechi hiyo Uwanja wa Emirates. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPEWA NAPOLI ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top