• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 31, 2019

  SAMATTA ATOA PASI YA BAO LA KWANZA KRC GENK YAITANDIKA MABAO 3-0 ANDERLECHT

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ametoa pasi ya bao la kwanza na kuonyeshwa kadi ya njano, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 3-0 katika mchezo wa ufunguzi wa Championship Round ya Ligi Daraja la Kwanza A Ubeligji dhidi ya Anderlecht Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alitoa pasi hiyo dakika ya 32 kwa beki Mdenmark, Joakim Maehle aliyefunga bao la kwanza dakika ya 32, kabla ya Nahodha huyo wa Tanzania kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 75.
  Mabao mengine ya Genk yalifungwa na washambuliaj Mjapan, Junya Ito dakika ya 55 na Mghana, Joseph Paintsil dakika ya 79.

  Championship Round inashirikisha timu sita ambazo pamoja na Genk, nyingine ni Club Brugge, Standard Liège, Anderlecht, Antwerp na Gent baada ya hatua ya awali, ijulikanayo kama Regular Season ambyo Genk imeongeza. 
  Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana amecheza mechi ya 147 kwenye mashindano yote na akiwa amefunga mabao 59 tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 114 na kufunga mabao 44 na kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili na Europa League amecheza mechi 24 na kufunga mabao 14.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Vukovic, Maehle, Dewaest, Lucumi, De Norre/Uronen dk74, Heynen, Berge/Piotrowski dk83, Malinovskyi, Ito/Paintsil dk59, Trossard na Samatta.
  Anderlecht; Didillon, Kara, Lawrence, Gerkens, Bolasie, Appiah, Santini/Amuzu dk64, Kums, Zulj/Trebel dk64, Obradovic na Verschaeren/Saelemaekers dk83.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOA PASI YA BAO LA KWANZA KRC GENK YAITANDIKA MABAO 3-0 ANDERLECHT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top