• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 11, 2019

  SIMBA SC YATAJA VIINGILIO MAPEMA MECHI NA AS VITA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba leo imetaja viingilio vya mchezo wake wa mwisho wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa ni Sh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.
  Manara amesema kwamba viingilio vingine ni Sh. 20,000 kwa VIPA A, Sh. 10,000 kwa VIP B na Sh. 100,000 kwa tiketi maalum za Platinums.

  Mchezo huo utakaoanza Saa 1:00 usiku, utachezeshwa na marefa wa Morocco, Noureddine El Jaafari atakayepuliza kipyenga na washika vibendera Hicham Ait Abbou na Yahya Nouali.
  Simba SC inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kutinga Robo Fainali, baada ya kupoteza mechi zake zote tatu za ugenini, 5-0 mara mbili dhidi ya Al Ahly nchini Misri na AS Vita mjini Kinshasa na 2-0 dhidi ya JS Saoura mjini Bechar. 
  Kwa sasa JS Saoura ndiyo inayoongoza Kundi D kwa pointi  zake nane baada ya kucheza mechi tano, ikifuatiwa na Al Ahly, AS Vita zenye pointi saba kila moja, wakati Simba SC inashika mkia katika kwa pointi zake sita.
  Wakati Simba SC ikimaliza na AS Vita mjini Dar es Salaam, Al Ahly watakuwa wenyeji wa JS Saoura Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria nchini Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATAJA VIINGILIO MAPEMA MECHI NA AS VITA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top