• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2019

  HAZARD AFUNGA BAO MECHI YA 100 UBELGIJI IKIICHAPA CYPRUS 2-0

  Eden Hazard akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 10 kabla ya Michy Batshuayi kufunga la pili dakika ya 18 Ubelgiji ikiwalaza wenyeji, Cyprus 2-0 katika mchezo wa Kundi I kufuzu Euro 2020 usiku wa jana Uwanja wa Neo GSP mjini Nicosia. Hazard amekamilisha mechi 100 za kuichezea Ubelgiji, huku mechi nyingine za kundi hilo jana Urusi iliikung'uta Kazakhstan 4-0 mjini Astana na Scotland ikaifunga 2-0 San Marino mjini Serravalle 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAZARD AFUNGA BAO MECHI YA 100 UBELGIJI IKIICHAPA CYPRUS 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top